1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Jacques Chirac wa Ufaransa yaahidi mchango wake Sudan ikubali majeshi ya Umoja wa mataifa Darfur

19 Septemba 2006

Kuna uwezekano serikali ya Sudan kukubali kuongezwa muda wa kuweko kikosi cha kiafrika cha wanajeshi wa kulinda amani katika jimbo lenye machafuko la Darfur magharibi ya Sudan. Muda wa kuweko kikosi cha Kiafrika Darfur unamalizika ifikapo tarehe 30 mwezi huu. Umoja wa mataifa unataka kuidhibiti hali ya mambo na wanajeshi 20,000 wa kulinda amani watakaoshika nafasi ya wanajeshi na polisi 7,000 kutoka nchi za kiafrika ambao kwa maoni ya Umoja wa matifa walishindwa kutuliza machafuko na mauwaji. Lakini rais wa Sudan Omar al-Bashir, jumamosi iliyopita alitamka tena kuwa kamwe hatakubali majeshi ya Umoja wa mataifa katika jimbo la Darfur. Rais wa Ufaransa Jacques Chirac, alisema kuwa atahamasisha serikali ya Sudan na Umoja wa matifa ili mpango huo ufanikiwe. Chirac alisema:

´´Mimi nitatoa wito kwanza kabisa kwa rais wa Sudan Omar al- Bashir ili akubali kikosi cha Umoja wa mataifa. Ni janga la kibinaadamu, tatizo la amani na ustawi. Linalotokea na litakalotokea kesho, ni jambo lisilokubalika. Pili nitatoa wito kwa Umoja wa mataifa ili uthibitishe nia yake ya kwenda nchini Sudan´´

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW