1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden aahidi ushirikiano mzuri kati ya Marekani na Afrika

3 Desemba 2024

Rais wa Marekani Joe Biden ameahidi ushirikiano wa kudumu kati ya Marekani na bara la Afrika utakaozingatia masharti ya Waafrika wenyewe.

Angola Luanda 2024 | Präsident Biden trifft Präsident Lourenco
Picha: Elizabeth Frantz/REUTERS

Biden ameyasema hayo wakati akikutana na rais wa Angola Joao Lourenco mjini Luanda, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kwanza Kusini mwa Jangwa la Sahara kama kiongozi wa Marekani. 

Lourenco amesema nchi yake Angola, inataka kufanya kazi na Marekani kuvutia uwekezaji wa kigeni na kuimarisha ushirikiano wa kiulinzi na kiusalama ikiwa ni pamoja na kufanya luteka za pamoja za kijeshi na ushirikiano katika maeneo ya Ghuba ya Guinea na kusini mwa bahari ya Atlantiki.

Rais Joe Biden wa Marekani yuko ziarani nchini Angola

Pamoja na  Lourenco kusifu uwekezaji wa makampuni ya Kimarekani katika sekta ya mafuta na gesi ya Angola, na miradi ijayo, afisa mmoja wa Marekani ameweka wazi kwamba mpango wa nchi hiyo ni kuwekeza zaidi katika mradi wa reli wa Lobito, unaolenga kurahisisha usafirishaji wa madini muhimu kutoka Afrika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW