1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Rais Joe biden kukutana na Stoltenberg

13 Juni 2023

Rais Joe Biden wa Marekani leo hii atamkaribisha ofisini kwake Katibu Mkuu wa NATO anaemaliza muda wake Jens Stoltenberg kwa mazungumzo.

Jens Stoltenberg alipozuru kambi ya kijeshi ya Marekani iliyoko Ujerumani ya Ramstein, Aprili 21, 2023.
Jens Stoltenberg anamaliza muda wake katikati ya mzozo unawakutanisha wanachama wa NATO na Ukraine dhidi ya Urusi.Picha: Heiko Becker/REUTERS

Mkutano huo unananyika katika kipindi ambacho ushindani unazidi kushika kasi wa kumsaka mrithi wake katika jumuiya hiyo ya kujihami ya mataifa ya Magharibi.

Mkutano wa awali na Biden ulipangwa Jana Jumatatu alasiri, lakini Ikulu ya White House ilitangaza kuwa umeahirishwa tena hadi leo Jumanne ili kupisha nafasi ya kufanyiwa tiba ya jino la Rais Biden

Mapema mwaka huu Stoltenberg, ambaye ameongoza NATO tangu 2014 kwa muda wake kuongezwa mara kadhaa, alionesha ishara ya kuweza kuendelea na dhamana yake hiyo akipata ridhaa endapo muda wake wa sasa utamalizika mwishoni mwa Septemba.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW