1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Biden na Xi wawekewa matumaini

12 Novemba 2023

Marais wa Marekani na China watakutana Jumatano pembezoni mwa mkutano wa kilele wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya bara la Asia na Marekani huko San-Fransisco

Marais wa Marekani na China walipokutana mwaka 2022 Nusa Dua,Bali, Indonesia
Rais Joe Biden na mwenzake wa China Xi Jinping walipokutana pembezoni mwa G20,Nusa Dua,Indonesia,Novemba mwaka 2022Picha: Saul Loeb/AFP/Getty Images

Rais Joe Biden wa Marekani na mwenzake wa China Xi Jinping wanatarajiwa kukutana,Jumatano wiki ijayo, pembezoni mwa mkutano wa kilele wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya bara la Asia na Marekani.

Mkutano huo unaofanyika katika mji wa San Francisco, Marekani,umekuja wakati ulimwengu ukikabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi huku shirika la fedha la kimataifa likikadiria kwamba ukuaji uchumi duniani unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 3 mwaka huu na asilimia 2.9 mwaka ujao.Soma pia: Waziri wa Fedha wa Marekani Janeth Yellen amesema wameweka msingi wa maandalizi ya mkutano kati ya rais Joe Biden na Xi Jinping wa China

Marekani na China ndio nchi zenye nguvu kubwa kiuchumi duniani,zikiwa ndio wazalishaji wa zaidi ya asilimia 40 ya bidhaa na huduma duniani. Mkutano kati ya viongozi hao wawili umeibua matumaini kwamba huenda ukapunguza mivutano ya kiuchumi iliyopo kati ya Marekani na China. Ingawa ikulu ya Marekani tayari imeshasema hakutarajiwi kufikiwa makubaliano ya aina yoyote.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW