Rais John Pombe Magufuli ameapishwa kwa muhula wa pili
5 Novemba 2020John Pombe Magufuli ameapishwa kufuatia ushindi wake kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 28.
Upinzani hata hivyo unadaia uchaguzi huwo ulikuwa na dosari, na udanganganyifu. Halikadhalika umeyakataa matokeo ya uchaguzi huo, na kutaka urudiwe tena, tume ya uchaguzi ivunjwe pamoja na kuitisha maandamano yasiyo na kikomo.
Soma pia: Magufuli aahidi kufanya kazi ya upinzani
Usalama uliimarishwa kabla ya kuanza kwa hafla hiyo ya kuapishwa Magufuli, na viongozi wa vyama viwili vikuu vya upinzani vya Tanzania, ACT-Wazalendo na CHADEMA, walishtakiwa kwa kuandaa maandamano kinyume cha sheria.
Mwishoni mwa wiki Rais Magufuli alisema hatowania muhula mwengine wa uongozi, huku kukiwa na wasiwasi kwamba chama tawala CCM, ambacho kimeshinda karibu viti vyote bungeni, huwenda kikajaribu kuongeza kikomo cha mihula miwili ya urais.