1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Kabila atangazwa mshindi wa uchaguzi DRC

10 Desemba 2011

Tume ya uchaguzi katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, imemtangaza rais wa sasa Joseph Kabila kuwa amechaguliwa tena kwa asilimia 49 ya kura .

kabila.jpg **FILE** President Joseph Kabila smiles during a meeting with former heads of state in Kinshasa, Congo in this Saturday, Nov. 4, 2006 file photo. Kabila appeared to have an insurmountable lead Tuesday, Nov. 14, 2006, in Congo's runoff election with nearly all the votes counted. (AP Photo/Schalk van Zuydam, FILE)
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya CongoPicha: AP Photo

Tume hiyo imesema kuwa mgombea wa karibu ya Kabila, kiongozi wa upinzani Etienne Tshsekedi , amepata asilimia 32 ya kura. Watu waliojitokeza kupiga kura katika nchi hiyo kubwa barani Afrika ni asilimia 59.
Tshisekedi amekataa matokeo hayo na kujitangaza kuwa rais mteule. Mahakama kuu katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo inapaswa hadi tarehe 17 mwezi huu kusikiliza rufaa za uchaguzi huo. Wakati matokeo yakitangazwa mjini Kinshasa jana Ijumaa, waungaji mkono wa rais Kabila walishangiria lakini wafuasi wa Tshisekedi wameeleza kuwa na hali ya wasi wasi. Ghasia wakati wa uchaguzi wa hapo Novemba 28 zimesababisha watu 18 kuuawa na kusababisha baadhi ya wakaazi kuikimbia nchi hiyo. Wachunguzi wa kimataifa wamesema kuwa uchaguzi huo umekumbwa na mapungufu kadha lakini wameshindwa kuuita wa udanganyifu. Matokeo ya awali ya uchaguzi wa bunge yanatarajiwa ifikapo katikati ya mwezi wa Januari. Rais ataapishwa Desemba 20.


Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo Etienne TshisekediPicha: picture-alliance/dpa
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW