Rais Kagame afanya uteuzi mpya wa mawaziri
5 Novemba 2019Matangazo
Mwanadiplomasia mkuu wa nchi hiyo, mwanasiasa mkongwe Vincent Biruta, atachukua nafasi ya Richard Sezibera ambaye hajaonekana hadharani kwa miezi kadhaa. Kutoonekana hadharani kwa Sezibera kumezusha uvumi kuwa huenda anaugua. Biruta amekuwa waziri wa mazingira tangu Agosti 2017 lakini alishikilia nyadhifa nyingine ikiwemo rais wa Seneti kati ya mwaka wa 2003 hadi 2011. Pia ni kiongozi wa chama cha Social Democratic - SDP ambacho kipo katika muungano na chama tawala cha Rwandan Patriotic Front - RPF kinachoongozwa na Kagame. Mabadiliko mengine yaliyofanywa yalimhusisha Patrick Nyamvumba aliyeteuliwa kuwa waziri wa usalama wa ndani. Alikuwa mkuu wa majeshi.