1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Kagame kukutana na Tshisekedi kupunguza mvutano

12 Machi 2024

Rais wa Rwanda amekubali kukutana na mwenzake wa Kongo ili kujadili hali ya usalama katika eneo lenye hali tete Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Rais wa Rwanda Paul Kagame , Rais wa Angola Joao Lourenco na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi mjini Luanda Julai 6, 2022,
Rais wa Rwanda Paul Kagame , Rais wa Angola Joao Lourenco na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi mjini Luanda Julai 6, 2022,Picha: JORGE NSIMBA/AFP

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Tete Antonio amesema imeamuliwa kuwa Rais Paul Kagame atakutana na Rais Felix Tshisekedi kwa tarehe itakayopangwa na mpatanishi.

Tamko hilo lilifuatia mkutano katika mji mkuu wa Angola Luanda kati ya Kagame wa Rwanda na Rais wa Angola Joao Lourenco ambae ni mpatanishi wa Umoja wa Afrika (AU).

Ofisi ya rais ya Rwanda imeonesha nia ya kushiriki upatikaji wa amai mashariki ya Kongo

Katika ukurasa wa X ambao ulifahamika kama Twitter awali, ofisi ya ofisi ya Rwanda imeandika "Wakuu wa Nchi wamekubaliana juu ya hatua muhimu za kushughulikia sababu za mzozo, na kudumisha haja ya mchakato wa Luanda na Nairobi ili kufikia amani na utulivu katika eneo hilo."

Marais Felix Tshisekedi kushoto na Paul Kagame

Mwishoni mwa Februari, ofisi ya rais wa Kongo ilisema kwenye ukurasa wake wa  X, kwamba Rais Felix Tshisekedi kimsingi ameoesha ukubali wake kukutana na mwenzake wa Rwanda. Lakini iliongeza kuwa "Felix Tshisekedi anadai kuondolewa kwa wanajeshi wa Rwanda kutoka katika ardhi ya Kongo, kusitishwa kwa mapigano na uasi wa M23 kabla ya kukutana na Paul Kagame."

Mkutano wa mwisho kati ya Kagame na Tshisekedi na matokeo magumu

Kagame na Tshisekedi walikutana mara ya mwisho katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa Februari 16 kando ya mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika, wakati wa "mkutano mdogo wa kilele" ulioandaliwa naLourenco.

Kulingana na vyanzo viwili vya kidiplomasia mjini Addis Ababa, mkutano huo ulikuwa wa mvutano mkubwa na ulimalizika kwa "kurushiana maneno makali"

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mapigano kati ya waasi M23 na vikosi vya Kongo yamepamba moto mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kuwafanya zaidi ya watu 100,000 kuyahama makazi yao. Kongo, Umoja wa Mataifa na mataifa ya Magharibi yanaishutumu Rwanda kwa kuunga mkono M23, madai ambayo serikali ya Kigali inayakanusha.

Soma zaidi:Tshisekedi akubali kukutana na Kagame

Baada ya miaka minane ya utulivu, waasi wa M23 walichukua tena silaha mwishoni mwa 2021 na kuyateka maeneo makubwa ya eneo la Kivu Kaskazini, ambalo linapakana na Rwanda. Mwishoni mwa mwaka 2023, Umoja wa Mataifa ulikadiria kuwa karibu watu milioni saba walikimbia makazi yao nchini Kongo, wakiwemo milioni 2.5 katika eneo la Kivu Kaskazini pekee.

Chanzo: AFP