1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Bolivia amshutumu Evo Marales kupanga mapinduzi

16 Septemba 2024

Rais Luis Arce wa Bolivia amtuhumu kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Evo Marales kwa kupanga njama ya mapinduzi

Bolivia La Paz | Rais Luis Arce
Rais Luis ArcePicha: Mateo Romay Salinas/Anadolu/picture alliance

Rais wa Bolivia Luis Arce,amemtuhumu rais wa zamani wa nchi hiyo, Evo Morales kwa kupanga njama ya mapinduzi kwa kuitisha maandamano na kuwekwa vizuizi mitaani,kama hatua ya kupinga ukosefu wa mafuta nchini.

Jana Jumapili rais wa zamani,Evo Morales aliidhinisha hatua ya kuanza kwa maandamano ya wafuasi wake wa kuanzia kesho Jumanne katika mji mdogo wa Caracollo na kuelekea mji mkuu La Paz.

Evo Morales kaachia ngazi

01:05

This browser does not support the video element.

Rais Luis Arce akihutubia jana alisema mwito uliotolewa na Morales utaishia kuwa mapinduzi dhidi ya serikali iliyopo madarakani.

Inaelezwa kwamba Morales anataka kugombea tena urais mwaka 2025 lakini mahakama zimemzuia na hivi sasa anajaribu kutumia wafuasi wake kuzilazimisha mahakama kupinduwa uamuzi huo.

Rais wa sasa Luis Arce na Evo Morales ni mahasimu wa kisiasa japo wote ni kutoka chama kimoja na wafuasi watalazimika kuchagua mmoja kati yao,kugombea mwakani.