1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUfaransa

Macron aitahadharisha Ulaya kuhusu makabiliano na Marekani

10 Februari 2026

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema hii leo kwamba Ulaya inapaswa kujiandaa kwa malumbano zaidi na Marekani na kuuchukulia mvutano kuhusu Greenland kama wito wa kutekeleza mageuzi ya kiuchumi yaliyocheleweshwa.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameuhimiza Umoja wa Ulaya kutobweteka na utulivu wa sasa baada ya mivutano na Marekani kuhusu Greenland
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameuhimiza Umoja wa Ulaya kutobweteka na utulivu wa sasa baada ya mivutano na Marekani kuhusu Greenland na kuitaka kupeleka mbele mageuzi ya kisektaPicha: Ludovic Marin/Pool/AP/picture alliance

Katika mahojiano yaliyochapishwa kwenye magazeti kadhaa ya Ulaya, Macron amesema Ulaya haipaswi kujidanganya na utulivu katikati ya mvutano na Washington kama mabadiliko ya kudumu licha ya kile kinachoonekana kama kumalizika kwa misuguano kuhusu Greenland biashara na teknolojia.

Amesema, utawala wa Trump umekuwa "ukiipinga waziwazi Ulaya" na unataka Umoja wa Ulaya kusambaratika.

Viongozi wa Ulaya watakutana mjini Brussels siku ya Alhamisi kwenye mkutano wa kilele ambapo watajadili hatua za kuimarisha uchumi wa umoja huo na kuifanya iweze kusimama kidete dhidi ya Marekani na China katika ngazi ya kimataifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW