1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Macron awasili Lebanon kuonyesha uungwaji mkono

17 Januari 2025

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliwasili Beirut siku ya Ijumaa katika ziara inayolenga kuunga mkono uongozi mpya nchini Lebanon.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Ludovic Marin/REUTERS

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliwasili Beirut siku ya Ijumaa katika ziara inayolenga kuunga mkono uongozi mpya nchini Lebanon.

Macron alikutana na waziri mkuu wa muda Najib Mikati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Beirut na anatazamiwa kukutana na Rais wa Lebanon Joseph Aoun na waziri mkuu mteule Nawaf Salam.

"Nimefurahi sana kuwa hapa, na nilitaka kutoa shukrani zangu kwa Waziri Mkuu kwa kuiongoza nchi kwa muda wote kwa maslahi ya kila mtu na ya Lebanon, na haswa katika miezi hii michache iliyopita, ambayo imekuwa migumu sana na hasa kutokana na vita," alisema Rais Macron.

Mikati amesema wamezungumza na Macron juu ya hali ya sasa na umuhimu wa kuendelea kusaidia Lebanon katika ngazi zote, kiuchumi na katika ujenzi mpya.Rais wa Lebanon amteua jaji wa ICJ kuwa waziri mkuu

Amesema Macron yuko tayari kuiunga mkono Lebanon na anakusudia kujadiliana na Benki ya Dunia jinsi ya kusaidia kulijenga upya eneo la kusini mwa nchi hiyo lililoharibiwa.

Macron pia anatarajiwa kukutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ambaye pia yuko Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW