SiasaAsia
Rais Macron wa Ufaransa aitembelea China
3 Desemba 2025
Matangazo
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anafanya ziara ya siku tatu nchini China ambako amewasili hivi leo, akilenga kujadili na viongozi wa nchi hiyo kuhusu biashara na diplomasia.
Kiongozi huyo wa Ufaransa anataka kuishawishi Beijing kuishinikiza Urusi kuelekea suala la kufikia makubaliano ya usitishaji vita na Ukraine.
Maafisa wa Ufaransa na China wanatarajiwa kwenye ziara hiyo kusaini makubaliano kadhaa katika sekta za nishati, chakula na usafiri wa anga.
Ofisi ya rais Macron imesema, kiongozi huyo atatetea juhudi za kuwepo soko huru lenye kuzingatia haki ya kibiashara.