1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Rais Macron atarajiwa kumtangaza Waziri Mkuu mpya

8 Januari 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatazamiwa hii leo kumchagua waziri mkuu mpya katika jitihada za kuitakasa serikali yake ambayo imekabiliwa na ukosoaji mkubwa.

Frankreich Macron und Borne in Paris
Rais Emmanuel Macron (kulia) akiwa na Waziri Mkuu Elisabeth Borne katika Ikulu ya Elysée mjini Paris: 19.07.2023Picha: Yoan Valat/AP Photo/picture alliance

Wiki liliyopita Macron alishauriana na viongozi muhimu ikiwa ni pamoja na waziri mkuu wa zamani Edouard Philippe na Waziri wa Fedha Bruno Le Maire.

Waziri Mkuu wa sasa Elisabeth Borne amekuwa katika wakati mgumu tangu mswada wa uhamiaji ulioshinikizwa na Macron kupigiwa kura bungeni mwezi uliopita baada ya kufanyiwa mabadiliko makubwa na yenye utata yaliyoshinikizwa na wapinzani wa mrengo wa kulia.

Soma pia: Mswada wa sheria ya uhamiaji wa Ufaransa wasababisha ghasia

Kulingana na mfumo wa utawala nchini Ufaransa, rais huamua jumla ya sera, lakini waziri mkuu ndiye anayewajibika kwa usimamizi wa serikali, na hii ikimaanisha kuwa mara nyingi huwajibishwa pale uongozi wake unapokabiliwa na msukosuko.

Hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanasema inawezekana pia Elisabeth Borne akasalia katika nafasi yake.