1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Macron wa Ufaransa yuko ziarani nchini India

17 Februari 2026

Ufaransa inataka kutanuwa ushirikiano wa kijeshi na India kwa kuingia mkataba wa mabilioni ya dola wa mauzo ya ndege za kivita

Rais Emmanuel Macron akiwa na mkewe Briggitte wakipokelewa nchini India
Rais Emmanuel Macron akiwa na mkewe Briggitte wakipokelewa nchini IndiaPicha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameanza ziara yake ya siku tatu  leo nchini India ambako atakutana na waziri mkuu wa India Narendra Modi.

Ziara hiyo inajikita kutazama zaidi ushirikiano katika sekta ya teknolojia ya akili mnemba  pamoja na uwezekano wa kufikia mpango wa mabilioni ya dola wa kuiuzia India ndege za kivita.

Ufaransa inatafuta kutanua ushirikiano wake wa kijeshi na New Delhi, huku mazungumzo yakitarajiwa kuhusu uwezekano wa kufikiwa mkataba wa mauzo ya ndege 114 za kivita za Kifaransa aina ya Dassault Rafale.

Waziri mkuu Modi amesema anaamini mazungumzo yake na rais Macron atakayekutana nae baade leo yataimarisha zaidi ushirikiano wa mataifa yao mawili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW