1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Mahamadou Issoufou ameshinda Tuzo ya Mo Ibrahim

8 Machi 2021

Rais wa Niger Mahamadou Issoufou ameshinda Tuzo ya Wakfu wa Mo Ibrahim ya 2020 kwa Mafanikio katika Uongozi wa Afrika. Na ameingia katika rekodi hiyo kama mshindi wa sita wa tuzo hio inayotambua uongozi bora Afrika.

Niger Symbolbild Fahne | Mahamadou Issoufou
Picha: Boureima Hama/AFP

Kamati ya tuzo hiyo katika taarifa yake imesifu uongozi wa kipekee wa rais Issoufou baada ya kurithi taifa lenye uchumi duni zaidi ulimwenguni, unaokabiliwa na changamoto ngumu zinazoonekana.

Katika kipindi chote cha kazi yake, Issoufa alijikita katika kukuza uchumi, kujitolea bila kutetereka kupigania utulivu wa kikanda na kikatiba pamoja na kupigania demokrasia ya Afrika. Soma zaidi Mo Ibrahim: Afrika yapiga hatua katika utawala bora

Festus MogaePicha: picture-alliance/ dpa

Akitangaza uamuzi huo, Festus Mogae, Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo hio ambaye pia ni rais wa zamani wa Botswana amesema nikimnukuu

"Katika masuala mazito ya kisiasa na kiuchumi, misimamo mikali na kuongezeka vurugu na majanga, rais Mahamadou Issoufou amewaongoza watu wake kwenye njia ya maendeleo. Leo, idadi ya Waniger wanaoishi katika umaskini imeshuka hadi asilimia 40 kutoka asilimia 48 katika kipindi cha muongo mmoja uliopita." Mwisho wa nukuu.

 

Mnamo 2011, Rais Issoufou alichaguliwa kidemokrasia baada ya utawala wa kijeshi wa miaka mingi nchini Niger. Alichaguliwa tena kwa muhula wa pili mwaka 2016 na kuachia madaraka baada ya kukamilika kwa muhula wake na kudhihirisha heshima yake kwa katiba.

Takwimu ya mwaka 2020 za Data za Wakfu wa Ibrahim kuhusu Utawala wa Afrika (IIAG) inasisitiza mafanikio ya Rais Issoufou, Katika miaka yake kumi kama Rais, Niger imefanya maendeleo katika maeneo mengi, pamoja na kuboresha sekta zote za Maendeleo ya Binadamu.

Aidha takwimu hizo zinadhihirisha kuwa mwisho wa muongo huo, Niger ilishika nafasi 28 kati ya nchi 54 katika faharasa ya Mo Ibrahim kuhusu utawala bora Afrika, na imetajwa kuwa kati ya nchi kumi za Kiafrika zilizoboreshwa zaidi katika kuimarisha fursa za kijamii na kiuchumi kwa wanawake. 

Mo-IbrahimPicha: Barefoot Live

Baada ya kamati ya Tuzo hio kujadilia na kutoa taarifa za mshindi, Mo Ibrahim amesema amefurahia uwamuzi uliotolewa wa kumtangaza mshindi Mahammadou Issoufou.

 

Mo Ibrahim amemtaja Issofou kama kiongozi mashuhuri ambaye amefanya kazi bila kuchoka kwa watu wa Niger, akikabiliana na changamoto ngumu za ukanda huo  kwa dhamira na heshima. Na anajivunia kuona Issoufou anatambuliwa kama mfano wa uongozi wa kipekee na anatumai uongozi wake utahamasisha vizazi vya uongozi wa Kiafrika. Soma Zaidi Rais Mstaafu wa Cape Verde Pires atangazwa mshindi wa Tuzo ya Mo Ibrahim .

Wagombea wa Tuzo ya wakfu wa Ibrahim wote ni Wakuu wa zamani wa Serikali au Serikali wa Afrika ambao wameondoka madarakani miaka mitatu iliyopita, wakiwa wamechaguliwa kidemokrasia na kutumikia muda wao uliowekwa kikatiba.

 

Chanzo: https://mo.ibrahim.foundation/news/2021/president-mahamadou-issoufou-wins-2020-ibrahim-prize-achievement-african-leadership

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW