Rais Marcos wa Ufilipino aimarisha usalama wa baharini
31 Machi 2024Hayo ni wakati mzozo kati ya Ufilipino na China ukiongezeka. Agizo hilo, lililosainiwa Jumatatu na kuwekwa hadharani leo, haliitaji China lakini linafuatiamfululizo wa makabiliano ya baharini na tuhuma za pande mbili kuhusu eneo linalogombaniwa la Bahari ya Kusini mwa China.
Rais Marcos ameapa kutekeleza hatua za kupambana na kile alichokitaja kuwa ni mashambulizi yasiyo ya halali, ya kulazimisha, ya uchokozi na hatari yanayofanywa na walinzi wa pwani wa China.
Beijing inadai kumiliki karibu Bahari yote ya Kusini mwa China, mfereji wa bahari unaoingiza zaidi ya dola trilioni 3 kupitia biashara ya kila mwaka ya safari za meli. Madai ya China yanaingiliana na yale ya Ufilipino, Vietnam, Indonesia, Malaysia na Brunei. Mahakama ya Kudumu ya Usuluhishi wa migogoro mnamo mwaka 2016 ilisema madai ya China hayana msingi wa kisheria.