1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Marcron aitembelea Syria

Josephat Charo
7 Julai 2026

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron yuko ziarani nchini Syria. Macron anatarajiwa kukutana na rais wa mpito wa Syria Ahmed al-Sharaa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kushoto, akilakiwa na waziri wa mambo ya nje wa Syria Asaad al-Shaibani alipowasili katika uwanja wa ndege wa Damascus.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kushoto, akilakiwa na waziri wa mambo ya nje wa Syria Asaad al-Shaibani alipowasili katika uwanja wa ndege wa Damascus.Picha: Ludovic Marin/AFP

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron yuko ziarani nchini Syria. Macron aliwasili Damascus jana Jumatatu kwa ziara ya kwanza ya mkuu wa nchi wa Ulaya Magharibi tangu mamlaka mpya ya Syria ilipochukua madaraka.

Macron alisema amekwenda Syria kuthibitisha tena kujitolea kwa Ufaransa kwa watu wa Syria, kwa Syria huru iliyoungana katika utofauti wake na yenye amani na majirani zake.

Macron na rais wa mpiti wa Syria Ahmed al-Sharaa waliutembelea msikiti maarufu wa Umayyad wa Damascus baada ya chakula cha jioni kabla mikutano rasmi inayotarajiwa kufanyika leo Jumanne.

Macron anatarajiwa kuondoka leo kurejea nyumbani Ufaransa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW