Rais mpya apatikana Somalia.
31 Januari 2009Matangazo
DJIBOUTI.
Kiongozi wa kiislamu mwenye mtazamo wa ukadirifu Sheikh Sharif Ahmed ameapishwa kuwa rais mpya wa Somalia baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika mjini Djibouti.
Sheikh Ahmed aligombea katika uchaguzi huo kwa niaba ya chama cha ukombozi wa Somalia -Alliance for Reliberation of Somalia.Alifanikiwa kupata kura nyingi katika raundi ya pili ya uchaguzi baada ya mgombea mwengine mzito, waziri mkuu Nur Hassan Hussein kujitoa.
Uchaguzi huo ulifanyika kufuatia kujiuzulu kwa rais wa hapo awali bwana Abdullahi Yusuf kutokana na mvutano mkubwa baina yake na waziri mkuu Nur Hassan Hussein.Bwana Abdullahi Yusuf alijiuzulu mnamo mwezi desemba mwaka jana.