1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLiberia

Rais Joseph Boakai aapishwa rasmi kuiongoza Liberia

23 Januari 2024

Rais mpya wa Liberia Joseph Boakai ameapishwa rasmi kuiongoza nchi hiyo kufuatia ushindi wake mwembamba dhidi ya nyota wa zamani wa soka George Weah katika uchaguzi wa Novemba.

Rais mpya wa Liberia Joseph Nyuma Boakai akiapishwa
Rais mpya wa Liberia Joseph Nyuma Boakai akiapishwaPicha: AP/picture alliance

Boakai, mwenye umri wa miaka 79, ameahidi kuliunganisha taifa hilo la Afrika Magharibi na kufufua uchumi wake.

Pia ametilia mkazo juu ya kuheshimiwa kwa utawala wa sheria, kupambana na ufisadi na kuleta matumaini mapya kwa raia wa Liberia kama moja ya vipaumbele vyake.

Hata hivyo, hafla hiyo ilimalizika ghafla baada ya Boakai, aliyekuwa amevaa mavazi ya kitamaduni ya Liberia, kuonyesha dalili za uchovu wakati alipokuwa akitoa hotuba yake.

Maafisa walilazimika kumuondoa jukwaani baada ya kushindwa kuimaliza hotuba yake.

Msemaji wa chama chake cha kisiasa ameweka wazi, uchovu wa Rais Boakai ulisababishwa na joto kali na wala haukuwa na uhusiano wowote na afya yake.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW