1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaArgentina

Rais mpya ya Argentina aanza kazi kwa onyo la kukaza mkanda

11 Desemba 2023

Rais mpya ya Argentina ameanza kazi rasmi akiwataka raia kujitayarisha kwa hatua kali za kukaza mkanda wakati akijaribu kuufufua uchumi ulioporomoka kabisa.

Rais mpya wa Argentina, Javier Milei, baada ya kula kiapo siku ya Jumapili (Disemba 10).
Rais mpya wa Argentina, Javier Milei, baada ya kula kiapo siku ya Jumapili (Disemba 10).Picha: Agustin Marcarian/REUTERS

Javier Milei aliwaambia wafuasi wake mara baada ya kula kiapo siku ya Jumapili (Disemba 10) mjini Buenos Aires kwamba amerithi nchi yenye uchumi mbaya kabisa kutoka kwa mtangulizi wake.

Milei alikiri kwamba serikali yake haina pesa yoyote, lakini aliapa kuchukuwa hatua za haraka kurejesha heshima ya taifa hilo la tatu kwa uchumi mkubwa katika Amerika Kusini.

Soma zaidi: Rais mteule wa Argentina ajadili hali ya uchumi na maafisa wa Marekani

Kiwango cha mfumuko wa bei kimefikia asilimia 140, ambapo asilimia 40 ya raia wanaishi kwenye umasikini.

Milei, anayefuata sera kali za ubepari, anatazamiwa kutekeleza ahadi yake ya kukata matumizi ya serikali, hatua itakayowaathiri mamilioni ya raia waliozowea kupokea ruzuku ya nishati na usafiri.