1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Rais mteule Donald Trump awateua wapambe wake

13 Novemba 2024

Trump ametangaza kuwa Bilionea Elon Musk, ataongoza idara mpya ya serikali ya ufanisi.

Trump amteua Elon Musk kuongoza idara mpya serikalini.
Trump amteua Elon Musk kuongoza idara mpya serikalini.Picha: JIM WATSON/AFP via Getty Images

Rais mteule Donald Trump ametangaza kuwa Bilionea Elon Musk, ataongoza idara mpya ya serikali ya ufanisi, pamoja na Vivek Ramaswamy ambaye hapo awali aligombea urais.

Trump amesema katika taarifa kwenye jukwaa lake linaloitwa "Truth Social” kwamba Musk na Ramaswamy watafungua njia kwa utawala wake, ya kuondokana na urasimu wa serikali, kupunguza kanuni za ziada, kuondosha ubadhirifu wa matumizi, na kuyarekebisha mashirika ya serikali kuu.

Musk, mwanzilishi wa Tesla na SpaceX na mmiliki wa mtandao wa X, alikuwa mfadhili mkuu wa Trump wakati wa kampeni zake za uchaguzi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW