1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump amemteua Mike Waltz kuwa mshauri wa Usalama wa Taifa

12 Novemba 2024

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua Mike Waltz kuwa mshauri wake wa masuala ya Usalama wa Taifa, vyanzo viwili vinavyolifahamu suala hilo vimeliambia shirika la habari la Reuters siku ya Jumatatu.

Donald Trump
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua Tim Waltz kuwa mshauri wake wa masuala ya Usalama wa Taifa.Picha: Julia Demaree Nikhinson/AP/dpa/picture alliance

Waltz, mfuasi kindakindaki wa Trump amekuwa mkosoaji mkubwa wa shughuli za China katika Ukanda wa Asia-Pasifiki na kuitahadharisha Marekani kujiandaa na mzozo mkubwa unaoweza kutokea kwenye ukanda huo.

Mwanajeshi huyo wa zamani amekuwa akizisifu sera za kigeni na mitizamo ya Trump huku akiikosoa vikali serikali ya Biden kwa namna ilivyowaondoa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan mwaka 2021.

Ushauri wa masuala ya usalama ni jukumu zito lisilohitaji kuidhinishwa na Seneti na Waltz atakuwa na jukumu la kumuarifu Trump masuala muhimu ya usalama wa taifa.

Trump aidha amemteua Seneta Marco Rubio kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Gazeti la New York Times limearifu.