1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSri Lanka

Rais mteule wa Sri Lanka aahidi mabadiliko ya kiuchumi

23 Septemba 2024

Rais mteule wa Sri Lanka Anura Kumara Dissanayake ameingia rasmi madarakani hivi leo akiahidi kuleta mabadiliko ya kimfumo katika taifa hilo.

Uchaguzi wa Sri Lanka - Rais wa Sri Lanka Anura Kumara Dissanayake
Rais mteule wa Sri Lanka Anura Kumara Dissanayake ameahidi mabadiliko ya kiuchumi baada ya kuchaguliwa rasmi.Picha: Sri Lankan President's Office/AP Photo/picture alliance / ASSOCIATED PRESS

Dissanayake amesema hayo baada ya kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi uliogubikwa na hasira za wapigakura dhidi ya hali ngumu ya uchumi.

Dissanayaka wa chama JVP mwenye umri wa miaka 55, amempiku mshindani wake wa karibu kwa zaidi ya kura milioni 1.3 na ameapishwa Jumatatu asubuhi akimrithi Rais Ranil Wickremesinghe aliyechukuwa madaraka baada ya mapinduzi ya umma ya mwaka 2022 yaliyouangusha utawala wa Rais Gotabaya Rajapaksa.

Rais huyo mpya wa Sri Lanka anakabiliwa na kibarua kigumu cha ukarabati uchumi wa nchi hiyo uliodorora pamoja na kufanikisha mpango wa uokozi wa mabilioni ya dola kutoka shirika la fedha la kimataifa IMF.

Viongozi wa India, Pakistan, China na visiwa vya Maldives wamempongeza Dissanayake kwa ushindi wake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW