1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Museveni akutana na kiongozi wa RSF mjini Entebbe

21 Februari 2026

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekutana siku ya Ijumaa na kiongozi wa wanamgambo wa RSF wa Sudan Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo.

Uganda Entebbe 2026 |  Museveni alipokutana na kiongozi wa Dagalo
Rais Museveni na kiongozi wa RSF Mohammed DagaloPicha: Uganda Presidential Press Unit

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekutana siku ya Ijumaa alasiri na kiongozi wa wanamgambo wa RSF wa Sudan Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo. Mkutano huo wa ngazi ya juu uliangazia kukomesha kwa mzozo unaoendelea nchini Sudan ili kurejesha amani na uthabiti kanda hii ya Afrika.

Vita  nchini Sudan ambavyo vimesababisha maafa na hasarakubwa vimedumu tangu Aprili 2023 kati ka RSF na majeshi ya serikali yanayongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhani.

Yaliyojadaliwa 

Katika majadiliano yao, rais Museveni alikariri msimamo wake kwamba vita vya Sudan  vyaweza kukomeshwa kupitia kwa mazungumzo badala ya siasa za mgawanyiko, kulingana na Ikulu ya Uganda.

Akielezea kuwa hoja hiyo hiyo ndiyo alimuhusia aliyekuwa rais wan chi hiyo Bashir akimshauri kuepukana na siasa zinazojikita katika ubaguzi na kutanguliza maslahi ya kisiasa.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekutana siku ya Ijumaa na kiongozi wa wanamgambo wa RSF wa Sudan Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo. Picha: Uganda Presidential Press Unit

Huku Museveni akisema kuwa Umoja wa Afrika ndiyo mwenye dhima kuu ya kukomesha mgogoro huo, Jenerali Dagalo alikubali kuwa Sudan kwa sasa inakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu inayohitaji kutatuliwa na wahusika katika mzozo huo.

Amekubaliana pia kwamba suluhu la amani ndilo linahitajika ili kukomesha mateso hayo kwa raia.

Wito wa Umoja wa Mataifa

Mkutano kati ya Museveni na Dagalo umefanyika wakati ambapo Umoja Mataifa inazidi kutoa shinikizo kwa pande zote mbili kusitisha mapigano.

Katika siku za hivi karibuni mauaji ya idadi kubwa ya watu yameripotiwa huku taarifa za mashirika ya kibinadamu yakielezea kuwa raia wa nchi hiyo wanakumbwa na hali mbaya zaidi ya baa la njaa pamoja na kukosa huduma muhimu za afya na elimu

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW