1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Museveni asema jeshi la Uganda lauwa ADF wengi

23 Septemba 2023

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema mashambulizi ya hivi karibuni ya angani dhidi ya waasi wenye uhusiano na kundi la Dola la Kiislamu huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yaliwauwa wanamgambo wengi.

Demokratische Republik Kongo | Soldaten von Uganda und DRC | Archivbild
Picha: Alain Uaykani/Xinhua/picture alliance

Na inawezekana yamemjumuisha mtengenezaji mabomu mashuhuri, Meddie Nkalubo.Hata hivyo, taarifa hiyo iliyotolewa na ofisi ya rais haikutoa maelezo ya kina kuhusu mashambulizi hayo ya anga ya Septemba 16 yaliyolenga maeneo ya waasi wa ADF, kundi la itikadi kali lenye kulaumiwa kwa machafuko ya mara kwa mara yakiwalenga raia wa Kongo walio makambini mashariki mwa taifa hilo.Taarifa ya Museveni inasema mashambulizi hayo ya angani yalilenga kambi nne za ADF zilizoko kati ya kilometa 100-150 kutokea kwenye eneo la mpaka wa Uganda. Uganda na Kongo zilianzisha operesheni za pamoja za kijeshi dhidi ya ADF mwaka 2021.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW