1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Museveni wa Uganda aongoza mkutano kuhusu Somalia

Lubega Emmanuel27 Aprili 2023

Viongozi, mawaziri na maafisa wa ngazi za juu kutoka mataifa yaliyo na askari wake nchini Somalia wanachunguza mpango wa kuwaondoa walinda amani nchini humo ifipako Desemba 2024

Uganda Kampala | Meeting zu Somalia
Picha: Ministry foreign affairs Uganda

Mkutano huu wa viongozi ni kilele cha vikao vya siku tatu ambavyo vimefanyika Kampala tangu siku ya Jumanne ambapo mawaziri wa ulinzi na masuala ya kigeni pamoja na wajumbe wa ngazi za juu Umoja wa Afrika na jumuiya ya wafadhili wamehudhuria. Washiriki ni kutoka kutoka mataifa ya Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Uganda na Somalia.

Soma Pia: Guterres asema Somalia ´inalipa gharama´ ya Mabadiliko ya Tabianchi

Katika vikao vyao, washiriki wamekubaliana kuendelea na utaratibu wa kuyaondoa majeshi yao wakisema kuwa ni hatua muhimu ili kuepusha kuzorotesha mafanikio waliopata kuhusiana na suala zima la amani usalama na uthabiti nchini Somalia. Katibu wa kudumu wa wizara ya masuala ya kigeni  Uganda Vincent Bagiire ndiye alisoma taarifa ya pamoja ya wajumbe.

Waziri wa mambo ya nje wa Uganda Vincent BagirePicha: Ministry foreign affairs Uganda

Awamu ya kwanza itakayomalizika tarehe 30 mwezi Juni mwaka huu inalenga kuwaondoa wanajeshi walinda amani  2,000. Kulingana na wadau, wana imani kuwa jeshi la Somalia sasa lina uwezo wa kuhakikisha, amani na usalama katika nchi hiyo. Hata hivyo, naibu katibu mkuu wa umoja mataifa anayeshighulikia usalama Dkt. Aisa Kirabo Kacyira amehimiza mataifa ya kigeni kuendelea kutoa misaada muhimu kwa jeshi la Somalia wakati majeshi ya Umoja wa afrika chini ya mpango ujulikanao kama ATMIS wakiondoka. Mkuu wa ujumbe wa Ulaya nchini Uganda Jan Sadek amekubaliana na mwito huo akisema kuwa misaada itakuwa nyeti katika kuleta amani ya kudumu Somalia na kuepusha maovu kama vile ugaidi kanda hiyo ya Afrika. Katibu wa kudumu wa wizara ya masuala ya kigeni wa Uganda Vincent Bagire amesema.

Soma pia: UN: Zaidi ya Wasomali 140,000 wakimbia makwako kutokana na msimu wa mvua za mafuriko

Changamoto kubwa inayokumba mpango huo imeelezewa kuwa uhaba wa fedha kuutekeleza kwani Umoja wa Afrika unahitaji kiasi cha dola milioni kumi na moja hivi kuundesha.

Hadi wakati wa kuandaa taarifa hii, mkutano wa viongozi wa mataifa hayo ulikuwa unaendelea akihudhuria pia rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud.