Rais Musharaf ataka mwili wa Bhutto uchunguzwe upya.
13 Januari 2008Matangazo
Islamabad. Rais wa Pakistan Pervez Musharraf ametoa wito wa kufukuliwa kwa mwili wa kiongozi wa upinzani aliyeuwawa Benazir Bhutto, kutokana na madai kuwa serikali yake inahusika na kifo chake. Katika mahojiano na gazeti la Newsweek la Marekani , Musharraf amesema anataka kuamuru kufanyika uchunguzi mpya wa mwili wa Bhutto, iwapo familia yake itakubali. Amekataa miito ya kufanyika uchunguzi wa umoja wa mataifa katika tukio hilo la kuuwawa kwa kiongozi huyo wa upinzani na kusisitiza kuwa maafisa wa Pakistan , wakisaidiwa na wataalamu wa Uingereza , wana uwezo wa kufanya uchunguzi wa kina.