1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Nana Akufo Addo amemfuta kazi mkuu wa tume ya uchaguzi

Daniel Gakuba
29 Juni 2018

Mkuu wa tume ya uchaguzi amefutwa kazi kwa tuhuma za utovu wa maadili na kushindwa na majukumu yake

Ghana Präsident Nana Addo Dankwa Akufo Addo
Picha: picture-alliance/Photoshot

Rais wa Ghana Nana Akufo Addo amemfukuza kazi mkuu wa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo, akimtuhumu kuwa na utovu wa maadili na kutoiweza vizuri kazi yake. 

Hayo yameelezwa na waziri wa habari wa nchini hiyo Mustapha Abdul-Hamid. Kufukuzwa kwa mkuu huyo Charlotte Osei na manaibu wake wawili kulitokana na mapendekezo ya tume maalumu iliyoteuliwa na Jaji mkuu wa Ghana, kuchunguza shutuma zilizokuwa zikiwakabili.

Tume hiyo ilipendekeza kuondolewa kwao kwa mujibu wa kifungu nambari 146(1)  cha katiba ya nchi kinachohusiana na mienendo na uwezo wa kazi.

Mwaka uliopita, ofisi ya rais ilisema imewasilisha kwa jaji mkuu, barua ya malalamiko ya baadhi ya wafanyakazi wa tume ya uchaguzi, ambao walimshutumu mkuu wa tume hiyo kutumia vibaya madaraka yake. Bi Osei alizikana shutuma hizo, na upinzani umekuwa ukisisitiza kuwa madai dhidi yake ni ya uongo.