1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Obama akutana na Netanyahu na Abbas

22 Septemba 2009

Rais wa Marekani Barack Obama leo anakutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas katika jitahada ya kufufua majadiliano ya amani ya Mashariki ya Kati yaliyokwama.

**CLARIFIES THAT PRESIDENT OBAMA IS SPEAKING** U.S. President Barack Obama addresses an audience at the Cairo University in Cairo, Egypt Thursday, June 4, 2009. Speaking in the ancient seat of Islamic learning and culture, and quoting from the Quran for emphasis, President Obama called for a "new beginning between the United States and Muslims", and said together, they could confront violent extremism across the globe and advance the timeless search for peace in the Middle East. "This cycle of suspicion and discord must end," Obama said in the widely anticipated speech in one of the world's largest Muslim countries, an address designed to reframe relations after the terrorist attacks of Sept. 11, 2001, and the U.S.-led war in Iraq.(AP Photo/Ben Curtis)
Rais wa Marekani, Barack Obama.Picha: AP

Mkutano huo wa pande tatu unaofanywa siku moja kabla ya kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hautazamiwi kuleta tija, hasa Israel ikiashiria tangu mwanzoni kuwa haipo tayari kubadilisha sera za ujenzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi.

Kwa maoni ya vyombo vya habari vya Israel, mualiko uliotolewa na Rais wa Marekani Barack Obama kwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa Israel ni ufanisi kwake kwani kabla ya kwenda mkutanoni mjini New York, hajakubali kusitisha ujenzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya yanayokaliwa na Israel . Wakati huo huo ofisi ya Netanyahu imesema, wakati wa mkutano huo wa pande tatu, Netanyahu atatetea sera za serikali yake kuhusu ujenzi wa makaazi hayo. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Danny Ayalon amesema:

"Umuhimu wa mkutano huo ni ukweli kuwa mkutano huo unafanyika. Jitahada thabiti za Marekani zimevunja nguvu msimamo wa Wapalestina."

Amesema, kama Mahmoud Abbas alifikiria kuwa ataitumia serikali mpya ya Marekani kuishinikiza serikali ya Israel ,basi sasa ametambua kuwa serikali hiyo haikushtushwa wala haikubadilisha msimamo wake.

Kuambatana na mpango wa amani maarufu kama "Road Map" uliokubaliwa mwaka 2003, Israel inatakiwa isitishe ujenzi wa makaazi ya walowezi katika maeneo inayoyakalia ikiwemo pia Jerusalem ya Mashariki. Na Rais wa Wapalestina alisisitiza hayo alipozungumza na waandishi wa habari.Amesema:

"Ikiwa Israel inataka kufanya majadiliano basi lazima isitishe ujenzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi na baadae ndio tutajadili masuala yaliyo muhimu."

Hamas wanaodhibiti Ukanda wa Gaza wanamlaumu kwa mara nyingine tena Rais Mahmoud Abbas kwa kutoheshimu ahadi alizotoa. Licha ya madai,kutaka ujenzi wa maeneo ya Wayahudi usitishwe moja kwa moja kabla ya kushiriki katika mazungumzo pamoja na waziri mkuu wa Israel, amekwenda New York kwa mazungumzo hayo hayo. Waziri mkuu wa zamani wa Palestina Ismail Haniyeh amesema huko Gaza, si PLO ya Mahmoud Abbas na wala si chama kingine chenye haki ya kudhuru mwongozo wa umma wa Palestina.

Mwandishi:C.Verenkotte/ZPR/P.Martin

Mhariri: M.Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW