1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKosovo

Rais Osmani: Kosovo i tayari kufanikisha uchaguzi kaskazini

2 Juni 2023

Rais Vjosa Osmani amesema Kosovo iko tayari kufanikisha uchaguzi mdogo mpya eneo la kaskazini lililokumbwa pamoja na mchakato wake wa awali kukumbwa na mzozo wa kisheria.

Osmani-Sadriu Vjosa | kosovarische Präsidentin
Picha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Rais Vjosa Osmani wa Kosovo amesema nchi yake iko tayari kufanikisha uchaguzi mdogo mpya katika eneo la kaskazini lililokumbwa pamoja na mchakato wake wa awali kukumbwa na mzozo wa kisheria.

Osmani ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari baada ya kukutana na Rais wa Serbia Aleksandar Vucic, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell kandoni ya Mkutano wa Kilele huko Moldova.

Mazungumzo hayo yalikuwa sehemu ya juhudi za kimataifa za kutatua mgogoro wa kaskazini mwa Kosovo, ambao ulizuka Jumatatu iliyopita na kusababisa wanajeshi 30 wa ulinzi wa amani wa Jumuiya ya Kujihami kujeruhiwa pamoja na waandamaji wa jamii ya Serb 52 pia kujeruhiwa baada ya kuzuka fujo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW