1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Paul Kagame wa Rwanda azuru Tanzania

27 Aprili 2023

Rais wa Rwanda, Paul Kagame leo amewasili nchini Tanzania kuanza ziara ya siku mbili katika taifa hilo la Afrika Mashariki na ambalo limekuwa likidumisha mahusiano yake na mataifa jirani.

Ruanda l Präsident Paul Kagame
Picha: Dan Kitwood/POOLAFP

Hii ni ziara yake ya kwanza nchini Tanzania tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipochukua wadhifa huo baada ya kifo cha mtangulizi wake, John Magufuli.

Rais Samia na Kagame wamekuwa na mazungumzo ikulu jijiji Dar es Salaam na kila mmoja amedokeza umuhimu wa kudumisha uhusiano mwema.

Rwanda imekuwa ikitegemea bandari ya Dar es Salaam kwa kusafirisha mizigo yake kutoka ng'ambo. Hadi mwaka 2021 Rwanda ilikuwa ikisafirisha tani milioni 1.366 kupitia bandari hiyo.

Moja ya malengo ya ziara ya Rais Kagame ni kuimarisha ushirikiano kupitia bandari hiyo ambayo imekuwa ikifanyiwa maboresho ili kukidhi mahitaji ya nchi jirani zinazoitegemea.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW