1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Putin aahidi kuharibu ndege za kivita itakazopewa Ukraine

28 Machi 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin amezionya nchi za Magharibi kuhusu kuipatia Ukraine ndege za kivita aina ya F16 akisema hatua hiyo haitobadili chochote katika uwanja wa vita.

Denmark | Rais Zelensky na Waziri Mkuu Frederiksen
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky (mbele) akiwa na Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen kwenye ndege ya kivita ya F16Picha: Mads Claus Rasmussen/Ritzau Scanpix Foto/AP/dpa/picture alliance

Putin amesema ndege hizo zina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia na hilo atalizingatia katika mikakati ya kijeshi.

Putin alinukuliwa na mashirika ya habari ya Urusi akisema kwamba ndege hizo zitalengwa kokote zilipo na zitaharibiwa kama vifaa vingine. Awali, Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alisema ndege hizo zinatarajiwa kuwasili nchini Ukraine katika miezi ijayo.

Soma pia:Zelensky ahimiza washirika wake kuharakisha mpango wa kuipa nchi yake ndege za kivita F-16

Ubelgiji, Denmark, Norway na Uholanzi ni miongoni mwa nchi ambazo zimeahidi kutoa msaada wa ndege hizo za kivita za F-16 kwa Ukraine, huku muungano wa nchi nyingine ukiahidi kutoa mafunzo kwa marubani wa Ukraine namna ya kutumia ndege hizo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW