MigogoroUkraine
Rais Vladimir Putin aitolea msharti Ukraine ili amalize vita
14 Juni 2024Matangazo
Kyiv imekataa masharti ya Moscow na imepinga kujisalimisha. Haya yanajiri kabla ya mkutano wa nchini Uswisi ambao Urusi haikualikwa.
Putin ameweka masharti hayo ya upeo wa juu kudhihirisha imani kwamba majeshi yake yana uwezo zaidi katika vita dhidi ya Ukraine.
Amesema ikiwa Ukraine itakataa kama hapo awali, basi watalibeba jukumu la kisiasa na kimaadili kutokana na kuendelea kwa umwagaji damu na kuongeza kuwa masharti kwa ajili ya kuanza mazungumzo yatakuwa tofauti.
Mshauri wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak ameyataja masharti ya Putin ni sawa na kupendekeza kwamba Ukraine ikubali kushindwa na kutia saini uhuru wake.