1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUrusi

Putin: Urusi bado ni mshirika muhimu kibiashara ulimwenguni

8 Juni 2024

Rais Vladimir Putin amesema Urusi inasalia mshirika muhimu wa kibiashara ulimwenguni licha ya kuelemewa na ongezeko la vikwazo vya magharibi.

urusi, St. Petersburg 2024 | Vladimir Putin akizungumza kwenye kongamano la kiuchumi
Rais Vladimir Putin asema Urusi bado ni mshirika muhimu wa kibiashara uliwenguni licha ya vikwazo vya magharibiPicha: Anton Vaganov/REUTERS

Putin amesema hayo jana Ijumaa kwenye Jukwaa la 27 la Kimataifa la Uchumi, SPIEF, mjini St. Petesburg na kuongeza kuwa Urusi ni miongoni mwa mataifa vinara kiuchumi, mbele ya Ujerumani akiangazia takwimu zinazozingatia uwezo wa manunuzi.

Kwenye hotuba mbele ya mamia ya wahudhuriaji, Putin alitoa wito wa kutanua ushirikiano katika masuala ya teknolojia na kutangaza matarajio yenye lengo la kuvutia wawekezaji zaidi kutoka nje.

Mataifa ya magharibi yameiwekea Urusi msururu wa vikwazo baada ya kuivamia Ukraine miaka miwili iliyopita.

Tangu kuwekwa kwa vizuizi hivyo vya kibiashara, Urusi imegeukia washirika wapya na hususan China, lakini pia India, Afrika na Amerika ya Kusini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW