1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Putin asikitishwa na wanajeshi wa Uturuki kuuwawa

Sylvia Mwehozi
5 Machi 2020

Rais Vladimir Putin ameelezea masikitiko yake kwa rais wa Uturuki Tayyip Erdogan kufuaatia wanajeshi wake 34 kuuwawa kwenye mashambulizi ya anga ya Urusi, akisema jeshi la Syria halikujua eneo walipokuwa wanajeshi hao.

Russland Moskau | Recep Tayyip Erdogan und Vladimir Putin
Picha: Reuters/P. Golovkin

Putin ameanza mazungumzo yake na Erdogan kwa kutoa pole kuhusiana na kuuwawa kwa askari wa Uturuki kwenye mashambulizi ya anga ya hivi karibuni. Akizungumza katika Ikulu ya Kremlin mjini Moscow sambamba na Erdogan, Putin amesema hali katika jimbo la Idlib ambako majeshi yao yanakabiliana katika vita iliyowaacha wakaazi karibu milioni moja bila makaazi, imekuwa ya kutia wasiwasi na ilihataji mazungumzo ya ana kwa ana.

"Mwanzoni mwa mkutano wetu, ningependa kutoa pole za dhati kuhusiana na vifo vya askari wako nchini Syria. Vifo vya watu daima huwa ni janga. Kwa bahati mbaya kama nilivyokueleza katika mazungumzo yetu kwa njia simu, hakuna mtu yeyote likiwemo jeshi la Syria ambaye lilijua walipokuwa wanajeshi wako", amesema Putin. 

Kwa upande wake rais Erdogan amesema anayo matumaini mkutano huo ulioitishwa na Putin utafikia makubaliano ya kupunguza mzozo. Afisa wa ngazi ya juu wa Uturuki amelieleza shirika la habari la Reuters kwamba viongozi hao wawili walikuwa na uwezekano wa kuafikiana juu ya usitishaji mapigano, baada ya wiki kadhaa za diplomasia kushindwa kusitisha mapigano baina ya Uturuki na vikosi va Syria vikiungwa mkono na Urusi.

Wafanyikazi wa shirika la kofia nyeupe wakiutoa mwili kwenye kijiji cha MaaretPicha: Getty Images/AFP/I. Yasouf

Umoja wa Mataifa ulisema mapigano hayo yamesababisha mgogoro mbaya wa kiutu katika vita yya syria vilivyodumu kwa miaka tisa sasa na kuwakimbizi raia mbali na makaazi yao huku mamia kwa maelfu wakiuwawa.

Naye mjumbe maalumu wa Marekani nchini Syria James Jeffrey, amezitolea wito nchi za Ulaya kuunga mkono juhudi za kijeshi za Uturuki jimboni Idlib. "Moja ya kanuni ambayo rais Donald Trump na bunge wanakubaliana ni kwamba lazima kuwepo na juhudi za pamoja, sio tu kwa Uturuki na Marekani bali kwa washirika wetu wa NATO, hususan wa Ulaya", alisema mjumbe huyo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Istanbul.

Nchini Syria kwenyewe, shambulio la anga kwenye kijiji kinachoshikiliwa na waasi, limepiga kwenye shamba moja ambako familia kadhaa zilizoyakambia makaazi yake zilikuwa zimejihifadhi ambapo watu 15 wameuawa wakiwemo watoto na wengine wamejeruhiwa. Wanaharakati wa upinzani wamedai kwamba ndege za kijeshi za Urusi ndizo zimekishambulia i´kijiji cha Maaret Musreen kaskazini magharibi mwa Syria.

Vyanzo:Reuters/afp

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW