1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Rais Putin awasili China kwa ziara rasmi

17 Oktoba 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amewasili nchini China leo Jumanne kukutana na rais mwenzake wa China Xi Jinping na kuhudhuria mkutano wa kilele .

Xi na Putin wanatarajiwa pia kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati.
Xi na Putin wanatarajiwa pia kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati.Picha: Sputnik/Mikhail Tereshchenko/Pool via REUTERS

Mkutano huo ulioandaliwa na China unalenga kujadili maendeleo yaliyofikiwa na China katika miradi ya miundombinu kimataifa.

Xi na Putin wanatarajiwa pia kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati.

Hapo jana Putin alisema pendekezo la China kuhusu mazungumzo ya amani na Ukraine linaweza kuwa msingi wa makubaliano ya amani. Ni kulingana na mahojiano aliyoyafanya na Televisheni ya China, ambayo yalichapishwa na ikulu ya Kremlin jana.

Putin aliishutumu pia Ukraine kwa kutokuwa na nia ya kushiriki mazungumzo hayo ya amani.

Lakini mara kadhaa serikali ya Kyiv imekuwa ikitoa sharti la kuondoka kwanza kwa vikosi vya Urusi katika ardhi yake, kabla ya kuanza mchakato wowote wa mazungumzo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW