1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Rais Putin wa Urusi asema vita vya Ukraine vitaendelea

21 Februari 2023

Rais wa Urusi Vlamidir Putin ameapa leo kuendelea na vita nchini Ukraine na kuyatuhumu mataifa ya magharibi kuwa yanauchochea zaidi mzozo uliopo kwa mataumini ya kuishinda Urusi.

Russland Präsident PutinRussland Präsident PutinRussland Präsident Putin
Picha: SPUTNIK/REUTERS

Katika hotuba ya kila mwaka ya hali ya taifa aliyoitoa muda mfupi uliopita mbele ya mabaraza yote mawili ya bunge na makamanda wa kijeshi,  Putin  amesema Moscow itatekeleza kwa ustadi mipango ya kijeshi na kutimiza malengo yake nchini Ukraine.

Amesema Urusi ilifanya kila inaloweza kuepusha vita lakini Ukraine ikiungwa mkono na mataifa ya magharibi ilikuwa inapanga njama za kuivamia rasi ya Crimea, eneo ambalo Moscow ililinyakua kutoka  Ukraine  mwaka 2014.

Kupitia hotuba hiyo ambayo yumkini imefuatiliwa kwa karibu na mataifa ya magharibi, Putin amesema kuishinda Urusi ni jambo lisilowezekana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW