1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Rajapaksa, mbioni kuondoka Sri Lanka

12 Julai 2022

Rais wa Sri Lanka, Gotabaya Rajapaksa anaelezwa kuwa katika mpango wa kulitoroka taifa hilo kwa kutumia boti ya doria ya jeshi la wanamaji baada ya kutokea tofauti kati yake na idara ya uhamiaji katika unjawa wa ndege.

Präsident von Sri Lanka Gotabaya Rajapaksa
Picha: Pradeep Dambarage/ZUMA Wire/dpa/picture alliance

Ikumbukwe tu Rais Rajapaksa alitoa ahadi kwamba atajiuzulu kesho Jumatano na kuweka uwanja wazi kwa ajili ya kufanikisha kukabidhi madaraka kwa amani, baada ya yale maandamano makubwa dhidi yake akitwishwa mzigo wa lawama kutokana na mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi nchini Sri lanka.

Kwa mkasa huo wa maandamano ya Jumamosi,kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73 aliyakimbia makazi yake rasmi huko Colombo kabla ya maelfu ya waandamanaji kuyavamia. Katika wadhfa wa uraisi Rajapaksa anakuwa na kinga ya kumzuia kutiwa mbaroni, na inaaminika anataka kuondoka nje ya taifa hilo kabla ya kutangaza kujiuzulu kwa kukwepa uwezekano wa kukamatwa.

Lakini akiwa katika uwanja wa ndege, maafisa uhamiaji waligoma kwenda katika eneo la uwanja huo linalotumiwa na watu mashuhuri maarufu kama VIP kumgongea muhuri wa ridhaa ya kusafiri, kutokana na kusisitiza kuwa anahofia kutoka hadharani kwa usalama wake, unaoweza kutishiwa na watumiaji wengine wa uwanja huo.

Kukesesha kwa Rais Rajapaksa na mkewe katika kambi ya kijeshi.

Waandamajai wakiwa nyumbani kwa raisPicha: AFP

Rais huyo na mkewe walikesha usiku kucha katika kambi ya kijeshi karibu na uwanja mkuu wa ndege wa Kimataifa wa Bandaranaike baada ya kukosa safari nne za ndege ambazo zingeweza kuwapeleka Umoja wa Falme za Kiarabu. Ndugu mdogo wa rais huyo, Basil ambae mwezi Aprili alijizulu nafasi ya uwaziri wa fedha, nae Jumanne iliyopita alikosa ndege akitaka kwenda Dubai, kwa namna hiyohiyo kutokana na kikwazo kutoka kwa maafisa wa uwanja wa ndege.

Basil mwenye uraia pia wa Marekani aliondolewa katika mpango wa safari zake pale alipojaribu kusafiri kwa kutumia kigezo cha huduma ya wafanyabiashara. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ufaransa AFP ni kwamba kulikuwa na baadhi ya wasafriki ambao walipinga Basil asiingie katika ndege hiyo kwa safari.

Ofisi ya rais ya Sri lanka iko kimya.

Hadi sasa hakuna taarifa yoyote kutoka katika ofis ya rais inayoeleza mahala alipo Rais Rajapaksa, lakini bado anasalia kuwa amiri jeshi mkuu na mamlaka yote yakiwa chini yake. Lakini chanzo kimoja cha juu cha kijehi kimesema wasaidizi wa rais huyo katika masuala ya usalama wanatafakari uwezekano wa kumundoa kiongozi huyo na wasaidizi wake kwenda nje ya nchi.

Boti ya jeshi la wanamaji ilitumiwa siku ya Jumamosi kumpeleka Rajapaksa na wasaidizi wake hadi mji wa bandari wa kaskazini mashariki wa Trincomalee, eneo ambalo baadae alisafirishwa kwa helikopta kurejeshwa uwanja wa ndege wa kimataifa siku ya Jumatatu.

Chanzo: Rais Rajapaksa wa Sri Lanka huenda akakimbia nchi

Pamoja na yote hayo, endapo atajiuzulu kama alivyoahidi, Waziri Mkuu Ranil Wickremesinghe atakuwa kaimu rais moja kwa moja hadi bunge litakapomchagua mbunge kuhudumu muhula wa urais, ambao utakamilika Novemba 2024.

Chanzo: AFP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW