1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruto atembelea kikosi cha polisi kilichoko nchini Haiti

Sylvia Mwehozi
22 Septemba 2024

Rais wa Kenya William Ruto siku ya Jumamosi aliwasili nchini Haiti na kudai kwamba uwepo wa kikosi cha polisi kutoka Kenya kupambana na magenge ya kihalifu, kumeimarisha hali ya usalama nchini humo.

Kenya | Ujumbe wa kikosi cha polisi wa Kenya kabla ya kuelekea Haiti
Rais Ruto akiteta na maafisa polisi kabla ya kuelekea HaitiPicha: REBECCA NDUKU/PRESIDENTIAL COMMUNICATION SERVICE/EPA

Rais wa Kenya William Ruto aliwasili nchini Haiti na kudai kwamba uwepo wa kikosi cha polisi kutoka Kenyakupambana na magenge ya kihalifu, kumeimarisha hali ya usalama nchini humo na kuruhusu raia waliokimbia makazi yao kurejea nyumbani.

Hata hivyo madai ya Ruto yanatofautiana na mtaalamu wa usalama wa Umoja wa Mataifa ambaye siku kadhaa zilizopita, alionya kwamba hali ya usalama katika taifa hilo imezidi kuwa mbaya, wakati magenge ya kihalifu yakizidi kupanua udhibiti wake katika taifa hilo la Karibiani. Kenya yaongeza maafisa 200 zaidi nchini HaitiMara baada ya kuwasili, Rais Ruto aliekelea moja kwa moja katika kambi ya kikosi cha polisi wa Kenya katika uwanja wa ndege na kukutana na maafisa waandamizi wa kikosi hicho, Haiti na Canada. Ruto ataelekea Marekani kuhudhuria mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW