1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Ruto atoa mwito wa mageuzi Baraza la Usalama

27 Septemba 2024

Rais William Ruto wa Kenya amesema mfumo unaosimamia usalama wa ulimwengu chini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unahujumu jitihada za kuimarisha amani kimataifa na ametoa mwito wa kufanyika mageuzi mapana.

Rais William Ruto wa Kenya
Rais William Ruto wa Kenya Picha: Frank Franklin II/AP Photo/picture alliance

Rais William Ruto wa Kenya amesema mfumo unaosimamia usalama wa ulimwengu chini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unahujumu jitihada za kuimarisha amani kimataifa na ametoa mwito wa kufanyika mageuzi mapana.

Soma: UNGA: Viongozi wahimiza upatikanaji wa suluhu ya mizozo

Ruto ametoa matamshi hayo alipohutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linaloendelea mjini New York. Amesema mfumo wa sasa unaolitenga bara la Afrika lenye mataifa 54 ndani ya Baraza la Usalama na ule unaowezesha taifa moja kutumia kura ya turufu kuyapinga maamuzi ya nchi yingine zote duniani haukubaliki.

"Ni lazima tutafute njia ya haraka ya kulifanya Baraza la Usalama kuwa lenye uwakilishi sawa, lenye ujumuishi, uwazi, la kidemokrasia, linalotimiza majukumu yake na lenye kuwajibika".

Kwenye hotuba yake Ruto pia amezungumzia haja ya kuyasaidia mataifa yanayoendelea kiuchumi kwa kuyasamehe madeni, kuyapatia mikopo nafuu na kuongeza uwekezeji katika miundombinu na sekta muhimu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW