1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Saied wa Tunisia akanusha madai ya ubaguzi

9 Machi 2023

Rais wa Tunisia Kais Saied amekanusha madai ya ubaguzi wa rangi baada ya kuwashambulia wahamiaji kutoka nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara.

ARCHIV | Tunesien | Präsident Kais Saied
Picha: Fethi Belaid/REUTERS

Matamshi hayo ya Saied yalipelekea watu kuachishwa kazi, kufurushwa wanakoishi na kushambuliwa. Ila sasa kulingana na ukanda wa video uliotolewa na afisi yake wakati wa mazungumzo na rais wa Guinea Bissau, Umaro Sissoco Embalo mjini Tunis kwamba, Waafrika walioko mjini Tunis ni "ndugu" wa Watunisia.

Wanaharakati wamkosoa rais wa Tunisia

Mnamo mwezi uliopita, Saied aliwaamrisha maafisa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na uhamiaji akidai bila kutoa ushahidi kwamba kuna njama ya kuhakikisha kwamba Waafrika weusi wanakuwa wengi katika idadi jumla ya watu nchini humo.

Rais Embalo ambaye ndiye mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS, amesema, hotuba ya Saied ilitafsiriwa vibaya. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW