1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Rais Sall atafuta muafaka juu ya terehe mpya ya uchaguzi

27 Februari 2024

Wadau wa siasa nchini Senegal wanaendelea na mazungumzo ya kutafuta muafaka juu ya tarehe mpya ya uchaguzi.

Rais wa Senegal Macky Sall
Rais wa Senegal Macky SallPicha: DW/AFP

Mazungumzo yaliyoitishwa na Rais Macky Sall wa Senegal, yenye nia ya kupata ufumbuzi wa tarehe mpya ya uchaguzi aliyouahirisha, yameingia siku yake ya pili huku mashirika ya kiraia yakijaribu kupata uungwaji mkono wa uchaguzi kufanyika ndani ya wiki kadhaa zijazo.

Senegal inapitia kipindi kigumu cha kisiasa ambacho hakijawahi kuonekana ndani ya miongo mingi, baada ya Sall kuahirisha uchaguzi saa chache kabla ya kampeni za uchaguzi huo uliokuwa ufanyike Februari 25 kuanza.

Soma pia: Matumaini ya urais ya Sonko wa Senegal yafifia

Muda wa Sall kuendelea kubakia madarakani unakamilika Aprili 2 na mashirika ya kiraia yakiongozwa na The Aar Sunu Eletion inayomaanisha tuulinde uchaguzi wetu, yanataka uchaguzi mpya ufanyike kabla ya Sall kuondoka madarakani.

Awali Rais Sall, alipendekeza muswada wa sheria ambao utatoa msamaha kwa waandamanaji wa kisiasa waliokamatwa kati ya mwaka 2021 na 2024.

Kulingana na makundi ya kutetea haki za binaadamu, zaidi ya watu 1,000 walikamatwa tangu mwaka 2021 wakati wa vurugu za kung'ang'ania madaraka kati ya Sall na kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW