1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Samia aungana na Chadema kuadhimisha siku ya wanawake

Veronica Natalis
8 Machi 2023

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyoandaliwa na tawi la wanawake wa chama kikuu cha upinzani Chadema.

Tansania | Opposition | Feier zum internationalen Frauentag
Picha: Emmanuel Ntobi

Hotuba ya Samia pamoja na mambo mengine iliendelea kutilia mkazo suala la maridhiano na kuijenga Tanzania. Hili linakuwa tukio la kwanza kushuhudiwa katika siku za hivi karibuni, kutokana hasa na mvutano mkubwa wa kisiasa ulioshuhudiwa miongoni mwa vyama hivyo vya siasa vyenye ushawishi mkubwa. Tanzania: CHADEMA yaanza kupokea ruzuku ya serikali

Rais Samia akiwasili Kilimanjaro na kupokelewa na viongozi wa ChademaPicha: Emmanuel Ntobi

Katika hotuba yake Rais Samia pamoja na mambo mengine,  ameendelea kutilia mkazo ajenda ya maridhiano na kutolipa kisasi na badala yake ametaka wafuasi na wanachama wa Chadema kusahau yaliyopita kwa kusonga mbele na kuendeleza ushirikiano wa kulijenga taifa la Tanzania. Anakiri kwamba yeye kama Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama chake cha CCM kualikwa katika shughuli za chama pinzania ni tukio la kihistoria.

Awali akizungumza katika maadhimisho hayo mwenyekiti wa chama hicho Taifa Freeman Mbowe, pamoja na mambo mengine ameendelea kutilia mkazo ajenda ya chama hicho ya kudai katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, pamoja na kumashauri Rais Samia kufanya maridhiano na vyama vingine vya siasa pamoja na makundi mengine ya watu, na katika hatua nyinge amegusia suala la wabunge wanawake 19 waliokuwa wanachama wa Chadema kwamba Chadema haitambui uwepo wao bungeni.

J3.08.03.2023 Chadema Samia - MP3-Stereo

This browser does not support the audio element.

Zaidi ya wanawake elfu tatu wakiongozwa kutoka Tanzania bara na visiwani ambao ni ambao wanaunda umoja wa baraza la wanawake Chadema Bawacha wamehudhuria sherehe hizo katika mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro. Maeneo mengine ya Tanzania yameadhimisha siku hii muhimu kwa kufanya maandamano na kubeba mabango yenye jumbe mbali mbali za kuhamasisha maeneo ya wanawake. Kauli mbiu yam waka huu inasema teknlojia na bunifu, chachu katika kuleta usawa wa kijinsia.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW