1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Samia Suluhu Hassan afanya ziara nchini Urusi

3 Juni 2026

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, yuko nchini Urusi kwa ziara ya siku tatu, ambapo leo alikutana na mwenzake Vladimir Putin, katika kipindi ambacho sifa ya nchi yake Magharibi imeathirika kwa kiasi kikubwa.

Urusi, Moscow 2026 | Vladimir Putin na Samia Suluhu Hassan
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kushoto) na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin (kulia) katika ikulu ya Kremlin mnamo Juni 3, 2026Picha: Ramil Sitdikov/AP Photo/picture alliance

Katika mkutano ulioonyeshwa moja kwa moja kwenye televisheni uliofanyika Kremlin, Samia alielezea ziara yake nchini humo kuwa ya kihistoria.

Kwa upande wake, Putin alisema amefurahi kumuona Samia nchini Urusi na akatoa wito kwa nchi hizo mbili kuongeza biashara kati yao.

Kwa sasa, biashara kati ya Tanzania na Urusi inakadiriwa kufikia zaidi ya dola milioni 307 za Marekani kwa mwaka. Mradi pekee wa pamoja wenye umuhimu mkubwa ni mgodi wa urani unaopangwa kujengwa, ambao umekuwa ukisubiri kutekelezwa kwa zaidi ya muongo mmoja.

Profesa wa zamani wa siasa kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, alieyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, amesema Urusi inaweza kufaidika na uungwaji mkono wa Tanzania, hata kama ni kwa  Tanzania  kujizuia kupiga kura katika kura muhimu za Umoja wa Mataifa kuhusu vita vya Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW