1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaeSwatini

Rais wa Taiwan afanya ziara nchini Eswatini

Saleh Mwanamilongo
2 Mei 2026

Safari hiyo ya kiongozi wa Taiwan ilisimamishwa kutokana na baadhi ya nchi za Afrika kuondoa ruhusa ya ndege yake kupita kwenye anga zao, hatua hiyo inadaiwa kusababishwa na shinikizo kutoka China.

Eswatini | Sikhuphe 2026 – Rais wa Taiwan, Lai Ching‑te, apokelewa na Waziri Mkuu Dlamini
Eswatini | Sikhuphe 2026 – Rais wa Taiwan, Lai Ching‑te, apokelewa na Waziri Mkuu DlaminiPicha: Taiwan Presidential Office/AFP

Rais wa Taiwan, Lai Ching-te, amewasili nchini Eswatini, baada ya ziara ya awali kufutwa.  Eswatini ni nchi mshirika pekee wa kidiplomasia wa Taiwan barani Afrika. Safari hiyo ya kiongozi wa Taiwan ilisimamishwa kutokana na baadhi ya nchi za Afrika kuondoa ruhusa ya ndege yake kupita kwenye anga zao, hatua hiyo inadaiwa kusababishwa na shinikizo kutoka China.

Katika ujumbe kwenye Facebook, Lai amesema ziara hiyo imefanikiwa baada ya kufanyika maandalizi ya siri, amesema lengo la safari yake kwenye taifa hilo la kusini mwa Afrika ni kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kilimo, utamaduni na elimu kati ya Taiwan na Eswatini.

Hata hivyo, China imekosoa ziara hiyo, ikidai kuwa Taiwan eneom linalojitawala ni sehemu ya China na juhudi zozote za kujitenga hazitafanikiwa. Eswatini ni miongoni mwa nchi chache duniani zinazoitambua rasmi Taiwan.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW