1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAlgeria

Rais Tebboune ashida muhula wa pili Algeria

14 Septemba 2024

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune ameshinda muhula wa pili kwa asilimia 84.3 ya kura katika uchaguzi wa wiki iliyopita, kwa mujibu matokeo ya mwisho yaliyotangazwa

Rais Tebboune ashida muhula wa pili Algeria
Rais Tebboune ashida muhula wa pili AlgeriaPicha: Aleksy Witwicki/Sipa/picture alliance

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune ameshinda muhula wa pili kwa asilimia 84.3 ya kura katika uchaguzi wa wiki iliyopita, kwa mujibu matokeo ya mwisho yaliyotangazwa. hata hivyo, matokeo hayo ni chini ya hesabu za makadirio ya awali yaliyopingwa na wapinzani.

Matokeo ya awali yaliyotolewa na mamlaka ya uchaguzi ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika, ANIE, wiki iliyopita yalimpa Tebboune karibu asilimia 95 ya uungwaji mkono, na hivyo kusababisha wagombea wengine kupinga matokeo hayo katika rufaa zao kwenye Mahakama ya Kikatiba.

Soma zaidi.Wagombea wawili wa uchaguzi Algeria wapinga matokeo mahakamani 

Rais wa mahakama hiyo ya kikatiba, Omar Belhadj, ametangaza hii leo katika televisheni na redio ya taifa matokeo rasmi yaliyompa ushindi Tebboune na kuwabwaga wapinzani wake wawili.

Hata hivyo, Ilitarajiwa kuwa Abdelmadjid Tebboune angelichaguliwa tena kwa muhula mwingine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW