1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Tinubu aahidi kushughulikia kero za raia wa Nigeria

5 Agosti 2024

Rais wa Nigeria Bola Tinubu ametoa wito wa kukomeshwa kwa maandamano makubwa ya kupinga ugumu wa maisha, akisema maandamano hayo yamegeuka kuwa ya vurugu.

Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu
Rais wa Nigeria Bola TinubuPicha: Nigerian Presidency/Anadolu/picture alliance

Rais wa Nigeria Bola Tinubuametoa wito wa kukomeshwa kwa maandamano makubwa ya kupinga ugumu wa maisha, akisema maandamano hayo yamegeuka kuwa ya vurugu.

Katika tamko lake juu ya maandamano hayo, Tinubu amejaribu kuwapoza waandamanaji akisema kuwa anaelewa uchungu na sababu zinazochangia maandamano na kwamba serikali yake iko tayari kusikiliza na kushughulikia kero za raia.

Aidha kiongozi huyo amewanyoshea kidole watu wachache aliowataja kuwa wana ajenda ya wazi ya kisiasa ya kulivuruga taifa. Hata hivyo matamshi yake yamekosolewa na baadhi ya watu ambao wanadai kwamba ameshindwa kuyazungumzia masuala muhimu yaliyochochea maandamano hayo.

Kumekuwa na ripoti za uporaji na uharibifu wakati wa maandamano pamoja na shutuma kwamba vikosi vya usalama vimetumia nguvu kupita kiasi. Shirika la kutetea haki za binadamu laAmnesty International limeripoti vifo vya waandamanaji tisa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW