1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Tinubu awasilisha bungeni miswada muhimu ya kodi

6 Desemba 2024

Rais wa Nigeria Bola Tinubu amewasilisha miswada minne ya mageuzi bungeni kama sehemu ya juhudi zake za kurekebisha mifumo ya kifedha na kodi katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika.

Bola Ahmed Tinubu
Rais wa Nigeria Bola Ahmed TinubuPicha: Sodiq Adelakun/AFP

Mageuzi hayo yameibua upinzani mkali, yakidhihirisha mvutano wa muda mrefu katika nchi hiyo iliyogawika mara mbili, eneo la kaskazini lenye Waislamu wengi na upande wa kusini wenye Wakristo wengi.

Miswada hiyo ya kodi inalenga kurahisisha ukusanyaji wa kodi na kuifanya nchi hiyo, inayotegemea mafuta kwa asilimia kubwa kama chanzo kikuu cha mapato yake, kuwa kivutio bora kwa wafanyibiashara wa ndani na wawekezaji wa kigeni.

Tinubu aahidi kushughulikia madai ya raia

Iwapo miswada hiyo itapitishwa na kuwa sheria, itapunguza ushuru unaotozwa watu binafsi na wanafanyibishara, na pia kupunguza kodi za mapato ya makampuni kutoka asilimia 30 hadi 25 katika muda wa miaka miwili ijayo.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW