Rais Trump apanga kulihutubia taifa Jumanne
23 Februari 2026
Rais Donald Trump wa Marekani anatarajiwa kutowa hotuba yake kwa taifa kesho Jumanne, ambayo huenda ikawa kipimo cha ujumbe unaotaka kufikishwa na chama chake cha Republican kwa wapiga kura wa nchi hiyo kuelekea uchaguzi wa katikati ya muhula.
Mwelekeo wa hotuba ya Trump ndio utakaoweza kuamuwa ikiwa chama hicho kitaungwa mkono kudhibiti bunge na baraza la Seneti nchini Marekani.Trump aongeza ushuru kimataifa kutoka asilimia 10 hadi 15
Kura za maoni zinaonesha majimbo mengi nchini humo yamepoteza imani na namna rais Trump alivyosimamia serikali katika muhula wake huu wa kwanza tangu aliporejea tena madarakani.
Kwa kiasi kikubwa hotuba ya Trump kwa taifa inatarajiwa kujikita kwenye masuala ya ndani ya Marekani lakini vitisho vya kuishambulia Iran kutokana na mpango wake wa Nyuklia, ambavyo amekuwa akizidi kuvitowa, huenda ni suala linaweza kuigubika hotuba hiyo hapo kesho.