1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Trump kutoa Hotuba ya Hali ya Taifa

24 Februari 2026

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kutoa hotuba ya kwanza ya Hali ya Taifa katika muhula wake wa pili hii leo, ambapo anatarajiwa kuelezea matokeo ya kile alichokifanya katika mwaka wake wa kwanza madarakani.

Donald Trump azuru China | Novemba, 2017
Rais Donald Trump wa Marekani alipozuru China. Trump anatoa hotuba ya hali ya taifa leo Jumanne huku China ikiwa ni moja ya nchi zilizoathirika na ushuru wa MarekaniPicha: picture-alliance/AP/TopPhoto

Trump atahutubia mabaraza yote mawili ya Bunge huko Washington, na hotuba hiyo huenda ikatoa mwangaza wa tathmini ya Trump kuhusu utendaji wa utawala wake kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula mwezi Novemba.

Anatoa hotuba hiyo siku chache baada ya Mahakama Kuu kufuta baadhi ya ushuru ambao ni sera muhimu kwa kiongozi huyo, na ambayo imewaacha njia panda washirika wengi wa kibiashara duniani.

Hotuba hii ya Hali ya Taifa pia inatolewa katika mwaka muhimu kwa Marekani, ambayo inaadhimisha miaka 250 tangu Azimio la Uhuru Julai 4, 1776.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW